Imezoeleka katika jamii zetu kuwa pale binti anapokaribia kuolewa basi wamama watamnunulia vyombo na mahitaji mengine ya muhimu ya nyumbani kama mashuka ili aweze kwenda navyo kwa mumu wake. Jambo hili ni jema na ni zuri, lakini vitu hivi vinapaswa vile vya pili na jambo la muhimu na la kwanza ni kutafuta na kujua je kama mke anapeleka nini kwenye ndoa yake? Vitu vitakavyosaidia kuijenga na kuisimamisha ndoa yake, vitu ambavyo huwezi kununua dukani wala kupewa na mtu yoyote. Vitu ambavyo havionekani kwa macho ndivyo hasa vinavyopaswa kuzingatiwa kwanza;
Nia ya kutunza na Kuhudumia
Mwanamke ana nafasi ya kutunza na kuhudumia(kiroho, kimwili na kihisia) wale wa nyumbani kwake. Anaweza kuamua kuihudumia familia yake na kuifanya kuwa bora na yenye furaha. Anapaswa kuweka mazingira ya nyumbani kuwa yenye amani, kusimamia mambo yote ya nyumba yake chini ya uongozi wa mume wake na kuwatunza watoto kwa upendo na kujali. Lazima uwe na nia ya kweli ya kufanya haya yote maana sio rahisi yanahitaji kujitoa kwa kweli na bidii pia.
Tabia Njema na Ushawishi Mzuri
Tabia ya mwanamke inapaswa kuwa nzuri ya kumfanya mumewe azidi kuheshimika na sio kumdhalilisha na kumuondolea heshima aliyokuwa nayo. Ushawishi wake kwa mume wake ni mkubwa kiliko ambavyo anaweza kufikiria hivyo ni muhimu sana akawa ni mtu mwenye tabia njema na ushawishi mzuri ili aweze kumjenga mume wake na sio kumbomoa. Tabia ya mke itafanya watu waithamini au waidharau familia nzima.
Moyo wa Utumishi na Upendo wa Kujitoa
Katika maisha ya sasa watu wanahimizana na kuhasishana kila mmoja kujiangalia kwanza yeye binafsi na kufanya kila analoweza kuwa na furaha bila kuangalia watu wengine. Lakini msingi wa ndoa nikuwa mume na mke wanakuwa mwili mmoja, hivyo huwezi kusema nataka furaha yangu tu maana tayari mu mwili mmoja. Unapoingia kwenye ndoa unapaswa kuwa na moyo wa utumishi, kuwa tayari kutumika kwa ajili ya familia yako na pia kuwa tayari kujitoa kwa ajili ya familia yako.
Unapokuwa katika njia panda hujui uchague nini kati ya mambo mawili mfano kazi jambo la muhimu kauangalia ni je ni jambo lipi litakuwa na mafanikio zaidi kwa familia yako na sio kujiangalia wewe binafsi.
chopra. 0721898979 - 0751898979
No comments:
Post a Comment