29 January 2011

How to Walk Like a Model


Instructions

  1. Choose shoes. Break in new heels or practice with a pair you've already worn in. You can start with 2-inch heels and work your way up. Put masking tape on the bottom of the heels to prevent them from slipping while you are walking like a model.

  2. Bring your shoulders back, and pelvic bone forward slightly to have the posture of a model. Keep your neck long, your stomach in, your butt tight and your chest out.

  3. Place one foot in front to begin the walk, putting it directly in front of the back foot, as if you are walking a tightrope. Keep your toes facing straight ahead. When done at a normal walking pace, this gives the model the swing that you see on the catwalk.

  4. Balance on the balls of your feet, instead of your heels. Always put the ball of your foot down first when you walk like a model.





5. Lengthen your normal stride by lifting your knees up a little higher when you walk and placing them out slightly more than you would normally. Let your arms swing naturally.


6.  Focus straight ahead when you walk like a model. Your head stays still as you walk, and your chin tilts up slightly. Your fingers curl ever so slightly, making your body look relaxed.


7.  Let your head be the last part of you that moves when you make your turnaround at the front of the catwalk (or your hallway).





chopra!!!


13 December 2010

Be A Good Kisser...

In this How To Be a Good Kisser post I’m going to explore the subject of how to be a good kisser by dealing with all of the things that you should not do. Whether you’re engaged in a loving emotional kiss or a very passionate sexual kiss the dos and don’ts are pretty much the same. The real difference is in the intensity of the kiss itself.




I think that one of best ways to learn how to be a good kisser is to study the things that you don’t like in other people’s kissing style. If you don’t have much kissing experience then you can simply take note of things that other people are turned off by. I’ll start with some of the kissing techniques that I myself hate and then add in those bad kissing habits that others have complained about.

Here are some things you do not want to do when you want to know how to kiss someone:
 
•Open your mouth too wide. In a kiss your lips should always be meeting the other persons, never surrounding them. I’m talking here about a full on open mouth kiss not the playful lip biting we all enjoy. I had a girlfriend once who just insisted on surrounding my lips with hers and it just grossed me out. Don’t do it!


•Pressing too hard. Once you’re in a kiss there is no need to try and continue moving towards the person you’re kissing, you’re not going to get any closer. Really.

•Too much tongue movement. This is big complaint about bad kissers. A french kiss is supposed to be a sensual express of love, not someone trying to beat your tongue into submission.

•Leaving your eyes open. Oh that’s just creepy. If you want to learn how to kiss, start with this tip: once you’re in range, close your eyes.

•Sucking too hard. Most of us enjoy a little sucking action during an expressive kiss but when my tongue feels like it’s in a vacuum chamber and blood vessels are about to burst you’ve gone too far.

•Lack of head movement. A good kiss should involve a little head movement as a kind of caress with your lips. When your partner’s moving their head and you’re not, you will make them feel uncomfortable and that you’re not into kissing them.

•This one is for guys only; women just ignore this, really, we don’t care. Guys, women don’t like when a kiss is an obvious attempt at getting sex. I know you’ve all seen the movie scene where the couple is tearing their clothes off 2 seconds into the kiss, but that rarely happens. If you try and recreate that scene you are most likely not only done for the night but forever with this woman. Here’s the approach you want to take: The “kiss” is it. It’s what you want and it’s all you want. It is the total expression of your feelings for this woman. Kiss her that way goodnight and then leave and she will not stop thinking about you for days.
Ok that’s my top list for things you do not want to do if you want to know how to be a good kisser. There is much more you need to learn about becoming a better kisser and I can’t possibly fit it all on this small website. If you really want to take your kissing to the next level you just take my number down there . I can’t promise it will make you a world class kisser but hey, you never know.
 
+254721898979
+254751898979
+254733898979

08 December 2010

How to Forget Your Ex...




Broken heart, depression, bitterness, painful longing; does this sound like you after your break up with your partner? The same feelings have been experienced by millions and billions of people all over the world and with such a large portion of people having the same experience why does it always seem so hard, why have we not understood the ways of the heart yet. In short why do we hurt so much and not learn how to forget your ex and get on with your life?
Some may say it is simply the way of love, other might say that it is a weakness of will and others may say it a necessary part of grieving over a failed relationship and perhaps all of them are right but none of these views help forget your ex so here are a few tips to help you move on and become a healthier, happier person.


1. Do Not Demonize Your Ex 
One thing that we are all tempted to do is to cast your ex in a bad light, to train yourself to hate them rather than want them back in a reactive exercise to crush any longing and pain by making them seem less desirable and unneeded. While you may envision yourself free of their influence because they will become detestable to you this creates more problems than it is worth and your new demonized feelings will be all mixed up with love making a tangle of emotions that can overwhelm, confuse and hurt you and any other relationships you may get involved with.

2. Reevaluate Yourself 
One issue with breakup is that of self worth. It does not matter who's fault it was or who left who in the end we all tend to see the relationship as a failure and in turn see ourself as a failure. Many men and women hung up on their ex partners tend to either wallow in self pity or self loathing and exaggerate everything in their emotional anguish making it impossible to forget your ex because you cannot sort out your own feelings for yourself. A Journey of self discover is often what sets many people free but how this is done is so varied and dependent on the person I cannot advice anything except that concentrating on your own feelings for yourself must happen before you start trying to work out how to forget your ex, in fact this process will help forgetting them immensely!

3. Do Not Be Irrational 
We all do it at some point, we get very drunk or go out and spend more than we can afford on clothes or food or anything else we enjoy to cover our problems. This can also manifest itself in terrible outings either trying desperately to get our ex back or to try to make them jealous. In the end they are irrational actions brought about by a need to take action of some sort. Simply put ... don't do it! They may seem like a good idea or clever at the time but they are a symptom of a heart in turmoil trying to work out how to forget your ex.

These are helpful hints to guide you back to a more healthy state of mind but if you want to know powerful psychological methods that can make you forget your ex in 24 hours.

+254721898979

+254751898979
+254733898979

22 September 2010

JIEPUSHE NA WANAOTAKA UACHANAE NA MPENZI WAKO ENDAPO UTAMFUMANIA NA MTU MWENGINE!!


HAINA HAJA UANZE MAISHA YA UPWEKE...


Fumanizi husababisha hisia zenye maumivu, hasira, kutokuaminiana, woga, aibu na kujilaumu. Lakini kufumaniwa au kufumania hakupaswi kuwa sababu wa kuwa mwisho wa ndoa yenu, ingawa kunaweza kuwa pia.

Baada ya fumanizi, inabidi ujitahidi kuelewa na kuweza kujenga tena ndoa yako, pengine sasa ikiwa ni ndoa imara zaidi. Hata hivyo hii inataka kujituma kwingi na uvumilivu na subira .

Ndoa inaweza kuendelea hata baada ya fumanizi kwa kutumia ushauri, kupeana muda na kushirikiana. Kuna ndoa ambazo zimeweza kudumu zaidi baada ya fumanizi kutokea.

Pale kutoka nje kwa mwanandoa mmoja kunapogundulika hupelekea hisia kali kwa wanandoa wote, mshtuko, aibu, kujilaumu, kujiona mkosaji, hasira kali na wasiwasi. Kutokana na hisia hizi zote mara nyingi wengi hufanya maamuzi yasiyo mazuri kama kutengana au kuachana kabisa.

Badala ya kufanya hivyo katika kipindi kile cha muda mfupi baada ya fumanizi, tunahitaji kuwa watulivu sana ili tuweze kuchukua hatua zinazofaa.

Kupata msaada: Kwa uzima na afya yako mwenyewe, tafuta msaada kutoka kwa familia, rafiki, mchungaji, shekhe au mshauri yeyote unayemwamini wewe na kujihisi huru kwake. Kuongea kuhusu hisia zako kwa wale unaowapenda sana itakusaidia wewe kupunguza nguvu za hisia za maumivu ya tukio hilo. Kuongea na watu wengine kunaweza kukupa wewe uwezo wa kuelewa zaidi hisia zako na kupata mtazamo mwingine kuhusu tukio.

Pengine aliyetoka nje inawezekana hatosheki katika mahusianao katika ndoa yake au hawajibiki vizuri katika ndoa. Au pengine hawezi kudhibiti mihemko yake.

Mabadiliko ya maisha kama kuzaliwa mtoto au upweke wa aina fulani, unaweza kuwa ndio sababu ya kutoka nje. Inabidi haya yatazamwe kabla mtu hajaamua lolote.

Kwa hiyo kujua sababu ya mwingine kutoka nje ni muhimu sana na hii inaweza kukupa ahueni, kwani unaweza kubaini kitu ambacho kinaonesha kwamba, kwako pia kuna matatizo.

Hatua zitakazokusaidia kujenga upya ndoa yako baada ya fumanizi ni nyingi. Lakini hizi ni baadhi tu ambazo kwa mazingira yanayokukabili, zinaweza kukusaidia.

Kuacha kutoka nje ya ndoa:
Hatua ya kwanza ni kwa mwanandoa kuacha tabia ya kutoka nje ya ndoa kiukweli. Mwanandoa anatakiwa kuacha kabisa mahusiano na mawasiliano na wapenzi wao wa nje, kujirudi kiukweli katika ndoa hakuwezekani bila kufanya hivyo.

Kukubali kuwajibika:
Kama umetoka nje ya ndoa, kuwa tayari kuwajibika katika vitendo vyako. Kama ulikuwa unadanganya, fikiri kuhusu matokeo ya vitendo vyako, fikiri kuhusu furaha uliyoiondoa kwa vitendo vyako, kubali kubadilika.

Onyesha nia ya malengo yako:
Kuwa na uhakika kuwa wote wawili mko tayari kujenga upya ndoa yenu. Inawezekana kuchukua muda kuondoa yote yaliyotokea na kuona kuwa mnaweza kuponya ndoa yenu tena. Kama wote mmefikia muafaka wa kujenga upya ndoa yenu basi ni vyema mjue kuwa itachukua muda, nguvu na kujitolea sana.

Onana na mshauri wa wanandoa:
Mtafute mshauri wa ndoa ambaye atakusaidia kujenga upya ndoa yako kama itakuwa inahitajika. Onana na mshauri wa ndoa ambaye alishawahi kukutana na kusaidia kutataua matataizo ya fumanizi. Mwepuke mshauri ambaye anaamini kumfumania au kufumania ndio mwisho wa ndoa yenu.

Kuchunguza tatizo:
Kufumania au kufumaniwa huzua matatizo katika ndoa. Chunguzeni kwa makini mahusiano yenu ili uweze kujua nini kilichosababisha au kilichopelekea kutoka nje ya ndoa na nini mfanye ili kuzuia kutoka nje ya ndoa tena. Epuka kutafuta msaada kwa watu ambao huwaamini na anajua hawawezi kukupa msaada mzuri kwa sababu itakuzidishia hisia za maumivu.

Kila mmoja apewe nafasi:
Kila mwanandoa anahitaji kupumzika kwa ajili ya kuondoa msongo na wasiwasi kutokana na tukio la fumanizi, hii ni kwa sababu huwa ni vigumu kusikiliza ushauri wakati mihemko iko juu sana.

Pata muda:
Epuka kujua undani zaidi kuhusu fumanizi la mwenzi wako kwa wakati wa mwanzoni. Ahirisha mjadala huo kwanza mpaka uzoee ile hali ya kumfumania mwenzi wako.

Fumanizi ni nini kwako?
Fumanizi sio kitu kimoja chenye maelezo au hali ya kueleweka kirahisi. Kuna aina nyingi za fumanizi. Kitu ambacho kinaweza kisikubalike kwa wanandoa fulani, kinaweza kukubalika na kuvumiliwa na wanandoa wengine kwenye fumanizi. Suluhu kwenye masuala ya fumanizi haifanani.

Kurudi katika hali ya kawaida baada ya fumanizi ni hali ambayo kiukweli ni ngumu sana, lakini inawezekana mmoja kuvumilia baada ya mmoja kutoka nje ya ndoa. Ushauri wa mambo ya ndoa utakusaidia kuliona tatizo hili kama matatizo mengine ya ndoa, jifunze jinsi ya kujenga tena ndoa yenye nguvu na mahusiano mazuri na epuka suala la kutalikiana, labda tu ama inabidi.

Kuelewa kwa nini mwenzi wako ametoka nje ya ndoa ni hatua muhimu katika kuweza kurejea tena katika ndoa na kuwa na furaha.

Kutoka nje ya ndoa huweza kutokea kwenye ndoa yenye furaha na isiyo na furaha na sababu zinatofautiana.

Baada ya mshtuko ule wa mwanzoni kuisha, zungumzeni kwa uwazi na upendo kuhusu kilichotokea, usijali ugumu katika kuongea au utakachosikia kuhusu tukio. fahamu kuwa unaweza kuhitaji msaada kwa mshauri au mtu yeyote unayemwamini ili uweze kuongea kwa uwazi zaidi.

Kama wewe ndiye uliyetoka nje ya ndoa unaweza kutengeneza ratiba kwa ajili yako wewe kuweza kujirudisha katika hali ya kawaida tena. Mara nyingi yule aliyetoka nje ya ndoa huwa na wasiwasi sana kuhusu tukio hilo. Kila mmoja anahitaji muda wa kuweza kujitibu mwenyewe.

Kwa watu wengine kusamehe ni suala gumu katika kujenga ndoa upya baada ya fumanizi.

Kusamehe siyo suala rahisi na la haraka. Inaweza kuwa kitu cha muda mrefu katika maisha, lakini kama umejitolea kwa mpenzi wako hili ni suala rahisi sana.

Mwisho wa ndoa au hapana ?
Siyo kila ndoa iliyoguswa na suala hili la fumanizi ni lazima imalizike kwa kutokuachana. Wakati mwingine kunakuwa na uharibifu mkubwa na wanandoa hawana budi kuachana na pia kama wanandoa hawako tayari kuwa pamoja tena.

Lakini kama wote mko tayari kujenga upya ndoa yenu, basi suala hili huwa rahisi sana na uhusiano utaendelea kuwa mzuri na wa amani zaidi.

USIPOMUHESHIMU MKEO... HAWEZI KUKUTHAMINI!!!!




Kuna wanaume ambao kwa kutokujua wanadhani mwanamke anachohitaji ni ‘fidia’ baada ya kuvunjiwa heshima, hivyo huwa wanawavunjia heshima wake zao na baadae kujitoza ‘fidia’ kwa kuwanunulia zawadi kubwakubwa wanawake hao.
Wanawake huwa wanapokea zawadi hizi, lakini hii haina maana kwamba ndoa itaendelea kuwa ya amani na upendo. Mwanamke hata kama atapewa dhahabu yote duniani, kama atajua kwamba mumewe hamheshimu, ni wazi kwamba hatakuwa na furaha ya ndoa. Miongoni mwa mambo sita ambayo mwanamke akiyakosa huhisi kutindikiwa na kukosa furaha ya uhusiano ni heshima.

Kama haki ya mwanamke hailindwi na mwanaume, hata kama kuna kitu gani, ndoa ni lazima itakuwa ni ya kubahatisha. Mwanume anapokuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yake, mwanaume anapomzuia mkewe kuamua masuala yake mwenyewe ambayo ni haki yake, kamwe mwanamke hawezi kuridhishwa na hayo na hata kama ndoa imejaa watoto wazuri wenye afya na akili na fedha nyingi zimeipamba nyumba yake.

Kama mwanaume ataonyesha kutojali kuhusu matamanio au ndoto za mkewe kamwe mwanaume huyo asitarajie kuwa mkewe atakuwa na upendo naye. Mwanamke huwa anatamani sana kuona mumewe anajali na kuyapa uzito matamanio au ndoto za mkewe. Kwa mfano mwanamke anapoonyesha kwamba, angependa kuanzisha shughuli labda ya biashara au wangependa wapate mtoto na mwanaume akaonyesha kutojali kuhusu matamanio hayo, kamwe mwanamke hawezi kutulia na kuwa na amani.

Kuna vitu au mambo ambayo mwanamke anayahitaji maishani, mahitaji hayo ni mengi yakiwemo yale ya msingi katika maisha na yale ya kawaida. Inatosha kusema kwamba, mwanamke anapogundua kwamba mumewe hajali juu ya mahitaji yake huwa hajisikii vizuri.

Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba mwanamke huhitaji heshima katika utashi na matamanio yake. Anapogundua kwamba utashi na matamanio yake havizingatiwi na mumewe hawezi hata mara moja kumkubali mume huyo. Kumkubali hapa ina maana ya kumkubali na kumtambua.

Hapo ndipo tatizo ambalo ni la upande wa pili huanza. Kwa maumbile mwanaume huwa anataka sana mkewe akimuonyesha kwamba anamthamini na kumtambua. Labda hii inatokana na ubabe wa asili wa wanaume ambapo kila wakati angependa kuona mwanamke akimgwaya na kuonyesha kwamba anamtambua kama ‘mwokozi’ wa aina fulani.

Kama mwanamke anataka kumfanya mumewe amsikilize na kujali matamanio na ndoto zake anachotakiwa kufanya ni kumuonyesha mumewe kwamba anamthamini na kumtambua. Kwa mfano mwanaume anapofanya jambo ambalo hata kama halina faida, lakini halina madhara, inabidi mkewe aonyeshe kuzitambua juhudi hizo na kuonyesha kwamba, mume huyo anajitahidi sana katika kufanya mambo yake.
Mwanaume anahitaji sana kuona mwanamke akimsifu kwa juhudi anazofanya, iwe ni za kitabia au za shughuli. Mwanaume anapokuwa na tabia nzuri, ni lazima mwanamke atafute kila njia ya kumuonyesha kwamba ameitambua tabia yake hiyo, kamwe asimuonyeshe kwamba juhudi anazofanya ni kupoteza muda. Pale ambapo mwanaume huonyesha heshima kwa mkewe kwa kuzijali ndoto na matamanio yake ya kimaisha, huhitaji sana kuonyeshwa kwamba heshima yake hiyo imepokelewa. Kwa kawaida mume anapotimiza wajibu wake lazima mke naye atimize wajibu wake.

Kuna wakati na karibu mara zote, mwanamke huwa anamlaumu mwanaume na mwanaume kumlaumu mwanamke kwa kila mmoja kudhani kwamba mwenzake ndio chanzo cha matatizo. Hii ni kwa sababu wote wawili hawajui namna nadharia hii inavyofanya kazi. Huyu anataka kuthaminiwa wakati hampi mwenzake heshima na huyu anataka kupewa heshima wakati hamthamini mwenzake.
Ili kuondoa kulaumiana huko inabidi kila mmoja ajue wajibu wake, kwani kama mmoja ataanza kumpa mwingine kile anachohitaji ni wazi huyu mwingine atajibu kwa kumpa mwenzake kile kinachomstahili mwenzake ambacho ni heshima.

chopra 0721898979 - 0751898979

18 September 2010

VUNJA MIGOGORO, JENGA UPYA NDOA YAKO NA UFURAHI NA MWENZAKO!!!




Wewe na mwenzi wako  mnakwazana kuliko kufurahishana, kuna mahaba kidogo sana yamebaki kwenye ndoa yenu lakini migogoro mingi. Kila njia ya kuboresha mahusiano yenu imeshindikana na hautaki kuendelea kuishi katika hali hii, unataka mabadiliko na furaha ya mwanzo irudi tena. Uwezo upo mokononi mwenu, unaweza kubadilisha ndoa yako na kuwa na ndoa mpya…na mwenzi wako uliyenaye kwa kufanya mambo kadhaa…
Kabili tatizo lako
Kubali kuwa ndoa yako ina hali mbaya na haipo sawa. Usipoteze muda na nguvu kuhuzunika na kujuta badala yake fikiria furaha na burudiko la moyo ambalo mnalikosa wewe na mwenzi wako kutokana na mifarakano kwenye ndoa yenu. Jambo hili liwe msukumo wa kuhakikisha unafanya jitihada zote ili uweze kuponya ndoa yako.
Bomoa ndoa yako iliyoharibika na uijenge upya
Wakati wana wa Israeli wanajenga ukuta wakati wa Nehemia, walipogundua kuwa wamekosea msingi waliubomoa na kuanza upya. Sababu umegundua kuwa ndoa yako imeharibika, bomoa na anza upya kuujenga msingi na kuisimamisha upya. Simamisha nguzo imara za kuishikilia isianguke tena ambazo ni Kusogea karibu na Mungu kwa maombi, kusoma neno lake na kuhudhuria kanisani; Kila mmoja wenu kuwa tayari kufanya kazi ya kuijenga ndoa yenu pamoja bila kulaumiana au kutegeana; na kuwa na muda wa pamoja kila siku ili kuimarisha uhusiano wenu.
Tubu
Badala ya kumlaumu mwenzi wako kwa matatizo ya ndoa yenu, kubali kuwa wote kwa pamoja mmechangia kuharibika kwake. Wajibika kwa matatizo yako yaliyosababisha kuvurugika kwa ndoa yenu. Kubali kuwa huwezi kumbadilisha mwenzi wako lakini unaweza kubadili mwenendo na matendo yako hivyo mwangalie Mungu akuwezeshe kuwa vile anavyotaka uwe. Kiri na tubu dhambi zako mbele za Mungu na umweleze jinsi gani unavyohuzunika dhambi zako zilivyoharibu uhusiano wako na Mungu pamoja na mwenzi wako. Omba msamaha toka kwa Mungu. Amua kuachana na matendo maovu na kutende mema kwa mume wako na watu wote.
Jadili makosa yenu na kufanya kazi kuyarekebisha
Kaeni chini pamoja na kila mmoja wenu kwa hiyari yake akirimakosa yake yaliyopelekea ndoa yenu kuharibika na kuomba msamaha kwa mwenzake na kutafakari pamoja nini kifanyike ili makosa hayo yasijirudie tena. Jitahidi kuwa ‘positive’ katika majadiliano yenu ili muweze kufikia muafaka ambao utaiboresha na kuijenga upya ndoa yenu. Hakikisha mnafanya kazi ya kuyakabili na kuyarekebisha makosa yenu kwa pamoja ili yasiweze kurudi tena.
Amua kuwa ‘positive’
Hata kama hisia zako kwa mwenzi wako sio nzuri, unaweza kuamua kuwasiliana kwa hali nzuri ‘positive’ ambayo hatimaye itaweza kuboresha hisia zako kwake. Tafuta kufanya mambo ambayo yataonyesha kuwa unamjali mwenzi wako, na ufanye hayo kila siku. Muombe Mungu akusaidie kuweza kuona mambo ambayo utayafurahia toka kwa mwenzi wako na jenga tabia ya kumsifia mara kwa mara. Kuwa na muda wa kuzungumza pamoja kuhusu mambo mbali mbali mnayoyapendelea wote.
Ponywa majeraha ya nyuma
Tafuta kuponywa majeraha ya kihisia yanayosababisha matatizo katika ndoa yako. Kama kuna kitu kilikuumiza zamani mfano kudhalilishwa kwa hali yoyote, kutengwa na wazazi, kukataliwa na mchumba n.k ambacho bado kinakusononesha ndani yako, tafuta namna ya kukuwezesha kupona kabisa ili uweze kuwa huru kuendelea mbele na maisha yako. Kama unaona ni ngumu sana tafuta msaada wa wataalamu wa saikolojia na ushauri ili uweze kuponywa kabisa bila kusahau kwenda mbele za Mungu ili kupata msaada.


Samehe
Amua kumsamehe mwenzi wako yale yote aliyokukosea na umweleze hivyo kuwa umemsamehe kabisa na upo tayari kusahau yote na kuanza upya. Usisamehe kwa kutegemea kitu Fulani, samehe kutoka moyoni.
Timiza mahitaji ya kila mwenzi wako
Zungumza na wenzi wako ujue ni nini hasa anahitaji toka kwako na hakikisha unayatimiza mahitaji yake kwa kadiri uwezavyo. Kuanzia mahitaji  ya kiroho, kihisia, kimwili na kiuchumi. Patikana pale anapokuhitaji, saidiana naye shughuli mbalimbali za nyumbali, nenda naye matembezi na pia uwe naye katika wakati anapokuwa na huzuni.
Kuwa Imara na mwenye msimamo
Kama mwenzi wako ametawaliwa na ulevi wa kupindukia au ni mgovi ambaye amefikia hatua ya kukupiga na kukutukana unapaswa kuwa jasiri na imara na kumweleza kuwa ni lazima abadili tabia yake au itakubidi  ueleze tatizo lako kwa wazazi au watumishi wa Mungu. Pata nguvu ya kukabiliana na hali hii katika maombi na kamwe usikae kimya pale unapokuwa na mwenzi anayekupiga na kulewa kupindukia. Tafuta msaada kwa wazazi wenu au wakubwa wenu huku ukiendelea kuomba mungu kwa bidii.

KIPI MUHIMU MWANAMKE ANAPASWA KWENDA NACHO KATIKA NDOA PINDI ANAPOOLEWA?



Imezoeleka katika jamii zetu kuwa pale binti anapokaribia kuolewa basi wamama watamnunulia vyombo na mahitaji mengine ya muhimu ya nyumbani kama mashuka ili aweze kwenda navyo kwa mumu wake. Jambo hili ni jema na ni zuri, lakini vitu hivi vinapaswa vile vya pili na jambo la muhimu na la kwanza ni kutafuta na kujua je kama mke anapeleka nini kwenye ndoa yake? Vitu vitakavyosaidia kuijenga na kuisimamisha ndoa yake, vitu ambavyo huwezi kununua dukani wala kupewa na mtu yoyote. Vitu ambavyo havionekani kwa macho ndivyo hasa vinavyopaswa kuzingatiwa kwanza;



Nia ya kutunza na Kuhudumia
Mwanamke ana nafasi ya kutunza na kuhudumia(kiroho, kimwili na kihisia) wale wa nyumbani kwake. Anaweza kuamua kuihudumia familia yake na kuifanya kuwa bora na yenye furaha. Anapaswa kuweka mazingira ya nyumbani kuwa yenye amani, kusimamia mambo yote ya nyumba yake chini ya uongozi wa mume wake na kuwatunza watoto kwa upendo na kujali. Lazima uwe na nia ya kweli ya kufanya haya yote maana sio rahisi yanahitaji kujitoa kwa kweli na bidii pia.
Tabia Njema na Ushawishi Mzuri
Tabia ya mwanamke inapaswa kuwa  nzuri ya kumfanya mumewe azidi kuheshimika na sio kumdhalilisha na kumuondolea heshima aliyokuwa nayo. Ushawishi wake kwa mume wake ni mkubwa kiliko ambavyo anaweza kufikiria hivyo ni muhimu sana akawa ni mtu mwenye tabia njema na ushawishi mzuri ili aweze kumjenga mume wake na sio kumbomoa. Tabia ya mke itafanya watu waithamini au waidharau familia nzima.
Moyo wa Utumishi na Upendo wa Kujitoa
Katika maisha ya sasa watu wanahimizana na kuhasishana kila mmoja kujiangalia kwanza yeye binafsi na kufanya kila analoweza kuwa na furaha bila kuangalia watu wengine. Lakini msingi wa ndoa nikuwa mume na mke wanakuwa mwili mmoja, hivyo huwezi kusema nataka furaha yangu tu maana tayari mu mwili  mmoja. Unapoingia kwenye ndoa unapaswa kuwa na moyo wa utumishi, kuwa tayari kutumika kwa ajili ya familia yako na pia kuwa tayari kujitoa kwa ajili ya familia yako.
Unapokuwa katika njia panda hujui uchague nini kati ya mambo mawili mfano kazi jambo la muhimu kauangalia ni je ni jambo lipi litakuwa na mafanikio zaidi kwa familia yako na sio kujiangalia wewe binafsi.


chopra. 0721898979 - 0751898979
      

12 September 2010

NIFANYEJE ILI KULINDA AJIRA YANGU? MAMBO 10 YA KUZINGATIA




Miezi kadhaa iliyopita niliongelea jinsi ya kupata kazi. Niliongelea mambo kadhaa ya kufanya au kutokufanya endapo umeitwa kwenye usaili(interview).
Pia kama utakumbuka wiki kadhaa zilizopita niliandika kuhusu mambo ya kufanya ili kuepuka migogoro makazini.Ukijiepusha na migogoro utakuwa umefanikisha jambo moja muhimu; kulinda ajira yako. Kama hupatani na wafanyakazi wenzako na kila kukicha wakuu wako wa kazi wanashinda wakisuluhisha migogoro yako, ni wazi kwamba siku zako zinahesabika.Utaipoteza ajira.
Leo naomba kuendeleza kidogo jinsi ya kulinda ajira yako.Kumbuka nyakati tulizonazo kiuchumi ni ngumu.Kuwa na ajira(ukiwa na uwezo ushauri wangu ni kwamba;jiajiri mwenyewe) ni muhimu.Ufanyeje ili kulinda ajira uliyonao?Unaweza kuzingatia mambo yafuatayo;
  • Fanya kazi yako vizuri: Hili la kwanza linaweza kuwa wazi.Umeajiriwa kwa sababu mwajiri wako anahitaji msaada kutokana na ujuzi ulionao.Unategemewa kufanya kazi zako kwa juhudi na maarifa.
    Zingatia maelekezo,sera na kila kitu kinachohusiana na kazi yako.Timiza wajibu wako.Kama kazi yako inakwenda sambamba na vitu kama “deadlines”,hakikisha unafanikiwa ipasavyo katika hilo.
  • Punguza kulalamika: Pamoja na kwamba waajiri wengi wanasema kwamba wana sera huru zinazoruhusu wafanyakazi kuelezea kero zinazowakabili nk,ukweli ni kwamba waajiri hao hao hawapendi kuwa na mfanyakazi au wafanyakazi wanaolalamika kupita kiasi.
    Kila inapowezekana,jitahidi kutatua matatizo madogo madogo unayokumbana nayo kazini bila kukimbilia kwa “wakubwa” ukiwa na lundo la malalamiko. Endapo ni lazima kulalamika,fanya hivyo huku ukiwa na mapendekezo halisi ya jinsi ya kukabiliana na tatizo husika.
  • Kuwa na siasa zisizofungamana na upande wowote: Kila mtu ana utashi wake katika siasa za nchi.Na kwa vile mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi,utashi wa kisiasa au vyama vya kisiasa unazidi.Pamoja hayo,hakikisha kwamba katika maeneo ya kazi,unakuwa au unaonyesha kuwa na siasa zisizofungamana na upande wowote.Kwa maneno mengine,usilete ofisini ushabiki wa kisiasa unaoonekana kuzidi mipaka au hata kuingilia utendaji wako.
    Lakini pia usionyeshe kwamba huelewi kinachoendelea nchini.Baadhi ya waajiri huutumia wakati huu kukagua watu wanaoelewa kuhusu sera mbalimbali za nchi,vyama vya kisiasa nk ili kujua nani au mfanyakazi yupi anastahili kushika usukani japo wa idara fulani.
    Kumbuka katika nchi nyingi zinazoendelea(Tanzania ikiwemo) mambo mengi(kama vile biashara na uwekezaji) yana uhusiano wa karibu sana na siasa za kiuchumi za nchi husika.Usikae kando sana.
  • Elewa na kukumbatia utamaduni wa sehemu yako ya kazi: Kila sehemu ya kazi ina “utamaduni” wake. Ukitaka kulinda ajira yako ni muhimu ukaelewa na kuukumbatia utamaduni(culture). Mifano ya tamaduni mbalimbali za sehemu za kazi ni mingi ikiwemo uvaaji(dressing code),utaratibu unaofuatwa pindi vitu kama misiba au harusi vinapotokea,nk.
    Hakikisha kwamba unaelewa “corporate culture” ya sehemu yako ya kazi na kwenda nayo sambamba.Usipofanya hivyo,utakuwa “tofauti”.Ukiwa tofauti ni wazi kwamba kila mtu pale kazi atakuwa anasubiri kwa hamu siku utakayoondoka.
  • Epuka umbeya: Hili niliwahi kuliongelea katika mbinu za kuepuka migogoro makazini.Lipo pia katika mbinu za kulinda ajira yako.Umbeya katika sehemu za kazi upo na utakuwepo.Hii ni hulka yetu binadamu ambayo wakati mwingine ni ngumu kuepukika.Pamoja na hayo,umbeya ni jambo ambalo huchangia sana watu wengi kupoteza ajira zao kwani umbeya makazini sio tu kwamba ni chanzo cha migogoro bali pia ni upotezaji mkubwa wa muda na pia kitu kinachoshusha morali ya wafanyakazi wengine.
    Kama unataka kulinda ajira yako,ni vizuri ukajiepusha na majungu na umbeya.Funga mdomo,ziba masikio.Fanya kilichokupeleka mahali pale;kazi yako.Umbeya uache nyumbani kwako na mtaani.
  • Jiendeleze kielimu na ki-ujuzi: Kupata kazi kusiwe mwisho wa kujifunza.Endelea kupiga msasa ujuzi au elimu yako kwa aidha kujisomea(siku hizi unaweza kusoma kupitia mtandaoni,kwa wakati wako).Inapotokea nafasi yoyote ya kujiendeleza kielimu,usiilazie damu.
    Unaweza kujiendeleza kielimu kwa kujisomea majarida au tovuti mbalimbali zinazohusiana na sehemu yako ya kazi. Kama upo umoja wa taaluma yako au kazi yako,hakikisha kwamba unakuwa mwanachama.Unapopata nafasi ya kukutana na wenzako katika taaluma moja,hakikisha kwamba unaelewa kinachoendelea katika taaluma yako.
  • Kuwa mwenye shukrani: Ni wazi kwamba hakuna binadamu ambaye anaweza kufanya kila kitu mwenyewe.Kila mtu anahitaji msaada fulani katika maisha.Hali ni hiyo hiyo katika sehemu za kazi.
    Ni muhimu kuwashukuru wale wote ambao wanakusaidia pale kazini kwako kwa namna moja au nyingine.Kimsingi wafanyakazi wenzako wote, iwe ni wafagizi,ma-messenger,katibu muhtasi nk,wanakusaidia kwa namna moja au nyingine.Washukuru kila mara unapopata fursa ya kufanya hivyo.
  • Kuwa na mtizamo chanya(positive attitude):Penye wengi,pana mengi.Yawezekana kazini kwako pakawa na mambo fulani fulani ambayo kimsingi hayapendezi.Kunaweza kuwa na mfanyakazi au wafanyakazi ambao ni “visima vya majungu”.Jiepushe nao na wakati huo huo hakikisha kwamba unakuwa na mtizamo chanya.
    Ukiwa na mtizamo chanya katika kila jambo,utapendwa na wafanyakazi wenzako na hata wakuu wako wa kazi.Watu walio na mtizamo chanya,wana nafasi nzuri zaidi ya kulinda ajira zao kuliko watu ambao wanaonekana wazi kuwa na msimamo hasi(negative attitude).
  • Kuwa mwaminifu: Bila shaka hili linajieleza.Uaminifu katika kazi na maishani kwa ujumla ni silaha nzuri katika mambo mengi.Bado nakumbuka jinsi Rais mstaafu,Benjamin Mkapa,alivyowaasa vijana katika suala zima la kuwa waaminifu ili kwenda sambamba na changamoto za maendeleo ya kiuchumi.Ni kweli kabisa.
    Hakuna mwajiri anayeweza kuvumilia mfanyakazi ambaye sio mwaminifu.Hakikisha unakuwa mwaminifu kwa kutumia vizuri muda wa kazi.Unapokwenda nje kwa ajili ya chakula cha mchana(lunch) hakikisha kwamba unarudi katika muda uliopangwa.Acha kuiba muda wa kazi kwa kupiga piga ovyo simu zako binafsi.Mifano ipo mingi sana katika hili.
  • Jipende na ujitunze: Ili uweze kulinda ajira yako ni wazi kwamba ni lazima uwe na afya nzuri.Kwa hiyo ni muhimu ukapata muda wa kutosha wa kulala,kula vizuri, fanya mazoezi mara kwa mara.Ukifanya hivyo utakuwa umejiweka katika mazingira mazuri ya kutimiza yote yaliyotajwa hapo juu.
Ukizingatia hayo niliyoyataja hapo juu ni wazi kwamba utakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kulinda ajira uliyonayo.Pamoja na hayo,yaweza kutokea ukaipoteza ajira uliyonayo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wako.Ni muhimu basi ukawa na “Plan B”.Linda ajira uliyonayo kwa hali na mali lakini usisahau kwanza;kuweka akiba ya kifedha benki au mahali pengine popote na pia kuwa na mbadala endapo ajira uliyonayo itatoweka.Siku zote lazima uwe umejiandaa.